Heade

AMTEMA MPENZI WAKE KWA KUWABAGUA WATU WEUSI


Henry Bolton and Jo MarneyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES / @JO_MARNEY
Image captionHenry Bolton na Jo Marney
Kiongozi wa chama cha UKIP nchini Uingereza Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.
Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.
Jo Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.
Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.
UKIP leader Henry BoltonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKiongozi wa UKIP Henry Bolton
Mwanajeshi huyo wa zamani alichukua usukani wa chama cha UKIP kama kiongozi mwezi Septemba, na kuwa kiongozi wa nne katika kipindi cha miaka 18.
Bw Bolton 54, alisema kuwa mwanamitindo huyo wa miaka miaka 25 alitimuliwa chamani mara moja baada ya chama kugundua kuhusu maoni yake.
Ujumbe huo ulitumwa wiki tatu baada ya wapenzi hao wawili kuanza uhusiano wao

No comments

Powered by Blogger.