Heade

MELI YA MAFUTA ILIYOKUA INATEKETEA KWA MOTO IMEZAMA BAHARINI


Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama bahariniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini
Meli ya mafuta ambayo imekuwa ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja hatimaye imezana, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China.
Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya Shanghai tarehe 6 Januari ambapo baadaye ilianza kusombwa kusini mashariki kwenda Japan.
Maafisa wa Iran sasa wanasema kuwa wahudumu wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa.

No comments

Powered by Blogger.