MAKAMO WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMEKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRELAND.
Makamo wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa nchi katika idara ya mambo ya nje na biashara wa Ireland Mhe Ciaran Cannon aliyeambatana na balozi wa Ireland nchini Tanzania kwenye jukumu maalum kwa ajiri ya Diaspora na maendeleo ya kimataifa.
Ambapo katika mazungumzo hayo maswala ya biashara na uwekezaji ndiyo yaliyotiliwa mkazo huku mazingira ya nchi hizi yakionekana kuruhusu kufanikiwa kwa mikakati hiyo.
Katika hatua hiyo Makamu w Rais ameelezea vifo vya akina mama kabla na wakati wa kujifungua na watoato wachanga na kuiomba serikali ya Ireland kupitia waziri huyo kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo hilo huku naye waziri wa Ireland akionyesha kuguswa na changamoto hiyo.
Aidha makamu wa Rais na waziri wa Ireland wamekubaliana katika suala zima la kuboresha elimu, mafunzo na kubadilishana ujuzi hasa katika masuala ya afya teknolojia na anga.
No comments