Heade

VIJANA WAMETAKIWA KUITUMIA VIZURI ELIMU YA UFUNDI



Vijana wametakiwa kuitumia vizuri elimu ya ufundi wanayoipata ili kuinua hali yao ya maisha na kuwa msaada kwa jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa sherehe ya mahafali ya 24  katika chuo cha maendeleo ya wananchi Tarime FDC, katibu wa CCM wilaya ya Tarime HAMIS  MKARUKA  KURA amesema elimu ya ufundi inazo fursa nyingi kwa vijana kama wakizingatia na kuitumia vizuri, wataleta maendeleo na mabadiliko makubwa katika jamii zao na Taifa hasa kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati na viwanda.

Aidha amesema anashangazwa kuona baadhi ya wananchi kuvamia na kuweka makazi katika eneo la chuo suala ambalo si zuri kwani eneo hilo bado linahitaji kuongezewa miundombinu ikiwemo mabweni na madarasa ili kuwa na uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi.

Naye makamu wa chuo Bi MASELE ameziomba halmashauri zote hapa wiliyani Tarime kukiunga mkono chuo hicho ili kupunguza baadhi ya changamoto zinazokwamisha maendeleo.


No comments

Powered by Blogger.