Heade

HIVYO ULIVYO UKITAMANI KUMUONA YESU UTAMUONA NAYE ATAKUHURUMIA NA ATABADILISHA HISTORIA YA MAISHA YAKO.


Katika maisha tunayoishi na mambo mbalimbali tunayoyapitia unaweza kufika wakati jamii ikakuona kuwa mtu usiyefaa na usiyestahili kuishi na watu na hata ukakoswa rafiki kabisa.
Kila unalolifanya utaona kuwa halifai na hata kama unajitahidi utende mambo mazuri kwa watu bado utahesabiwa kasoro nyingi na yote unayoyafanya kuonekana si kitu.

Inafikia wakati unajisikia kumwona Yesu katika maisha yako hata pengine unatamani uende kanisani uungane na watu wanao mwomba Mungu lakini kutokana na maneno yanayosemwa juu yako na jinsi jamii inavyokuchukulia unasita kwenda kanisani na pia huenda umeamua na ume enda kanisani lakini minong’ono ya kukubeza imekuwa mingi ,umekuwa kionyesho kila unako pita kwamba Yule naye anaenda kanisani, nikwambie usiogope ufuate moyo uliokusukuma kumwendea Yesu.

Ukisoma biblia katika kitabu cha Luka 19:1-10 utaona habari za Zakayo , Zakayo alikuwa  mtu wa cheo mtoza ushuru na tajiri na biblia inasema alipenda kumwona sana Yesu aliposikia anapita mahali pale alipokuwa lakini kutokana na wingi wa watu alishindwa kumwona maana Zakayo alikuwa mfupi hivyo akamua kupanda juu ya mti ili iwe rahisi kumwona Yesu na Yesu alipofika akamwona Zakayo juu ya mti akamwambia Zakayo shuka upesi leo imenipasa kupumzika nyumbani mwako.
Zakayo akashuka upesi akampeleka Yesu kwake ,watu wengi wakaanza kunung’unika wakisema mbona huyu anaingia na kukaa na wenye dhambi maaana Zakayo hakuwapendeza wengi na walikosana na watu wengi kwa kazi yake ya kukata ushuru.
Wakati ule ule Zakayo akamwambia Yesu, “BWANA, kama kuna mtu yeyote niliyemdhurumu mali yake nitamrudishia mara nne” na akaingia kwenye hazina yake akatoa vyote alivyowadhurumu watu na kuwarudishia.
Hivyo nikwambie kwamba pamoja na jinsi watu walivyokuwa wana mchukulia Zakayo kuwa si mtu mwema na hata kunung’unika walipo ona Yesu ameingia ndani mwake ni kwa sababu hawakujuwa kuwa ingawa mtu anaweza kuwa mtenda mabaya lakini akiamua kukutana na Yesu historia yake hubadilika na Yesu yuko kwa ajili ya kuwabadilisha waliokuwa waovu kuwa watu wema, waliokuwa wanawaumiza watu ,kuwa msaada wa watu wengine.
Usijihesabie hatia hata ukashindwa kutii sauti na msukumo unao usikia ndani yako wa kwenda mbele za BWANA ,kutaka kukutana na Yesu, kubali kukutana na Yesu anayebadilisha historia ya mtu  naye ataibadilisha historia ya maisha yako.
Zakayo angejihesabia hatia na kusikiliza minong’ono ya watu iliyokuwa ikipinga kuwa hana haki ya mwana wa Mungu kuingia  nyumbani kwake  huenda angepitwa na Yesu lakini hakusikiliza watu wanasema nini alikazana na kutaka sana kumwona Yesu na baada ya kukutana na Yesu akapata rehema na maisha yake yakabadilika.
Yesu yuko kwa  kwa ajili ya wote wasionekana kuwa kitu mbele za watu na kuwafanya kuwa wa thamani tena, mkimbilie Yesu ataibadilisha historia ya maisha yako.
jamesmtiba@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.