Heade

USIKAE KIMYA UNAPOPOKEA TAARIFA MBAYA JUU YA MAISHA YAKO MWITE MUNGU ATAKUSAIDIA


Natumaini kuwa unaendelea vizuri mpenzi msomaji wa masomo haya mazuri yanayo endelea kupitia blog hii na Mungu anaendelea kukusaidia kuyaelewa,  kukubariki na kuyabadilisha maisha yako .
Unatokea wakati unapokea taarifa mbaya ambazo zinakuumiza moyo kukukosesha raha na hata kukufanya ukate tamaa.

Taarifa hizi zinaweza kutoka kwa ndugu, jamaa,rafiki, kwa watu mbalimbali wenye uhusiano na sehemu ya maisha yako inayoweza kutolewa taarifa na nyingine  kwa adui zako.Mfano unaweza kupokea taarifa za vipimo vya madaktari zinazokuwambia ugonjwa ulio nao hauwezi kupona utakufa.

Pengine umesikia mtu fulani ama watu unaofahamiana nao wametoa taarifa mbaya juu yako ,wamesema utakufa masikini, wamesema huwezi kujenga kwako utaishia nyumba za kupanga mpaka uzeeni, hautaoa  au utazeeka bila kuolewa ;usikubali kukaa kimya. 
Taarifa mbaya kama hizo inakubidi uzikabili kwa kuzikataa kwa maombi  na Mungu wa mbinguni wa huruma na  mwenye rehema atakusaidia.
Ukisoma biblia katika kitabu cha Isaya 38:1-9, utaona habari za Hezekia.Siku hizo Hezekia aliugua akawa katika hatari ya kufa;na Isaya nabii ,mwana wa Amozi,akaenda kwa mfalme akamwambia,BWANA asema hivi, tengeneza mambo ya nyumba yako maana utakufa wala hutapona.Basi Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA ,kumbuka haya nakusihi kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Ikawa neno la BWANA likamjia Isaya,kusema enenda ukamwambie Hezekia, BWANA Mungu wa Daudi, baba yako asema hivi,mimi nimeyasikia maombi yako ,nimeyaona machozi yako ,tazama nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. Nami nitakuokoa wewe na mji huu na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu. Jambo hili liwe ishara kwako itokayo kwa BWANA, ya kuwa BWANA ,atalitimiza jambo hili alilolisema. Tazama nitakurudishia nyuma kivuli madaraja kumi ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara,ambayo limekwisha kushuka.
 Hayo ndio maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda alipokuwa hawezi naye akapona ugonjwa wake.
Mpenzi msomaji, unaona baada ya Hezekia kumlilia Mungu akapata rehema na akaongezewa miaka mingine 15 ya kuishi. Kama Hezekia angenyamaza kimya asichukue hatua ya kuzikabili taarifa mbaya alizopewa hakika angekufa. 
Usikubali kukaa kimya unapo pokea au sikia taarifa mbaya juu ya maisha yako, watu wako na mali zako zikabili taarifa mbaya kwa kumwomba Mungu na Mungu atakusaidia. Wapo watu wengi waliopokea taarifa mbaya juu ya maisha yao lakini walipomlilia Mungu mambo yalibadilika .
Wapo walio ambiwa hawatamaliza mwaka watakufa, lakini mpaka leo imepita miaka mingi na bado wanaishi kwa sababu walizikataa taarifa za kifo chao kwa maombi.
 Waliambiwa watakufa bila kujenga lakini  wamejenga wana miji yao na wamewapangisha wengine, hii ni kwa sababu walizipinga taarifa mbaya.
Wengine waliambiwa wakufa masikini lakini leo wana utajiri mkubwa kwa sababu walizikabili taarifa mbaya kwa maombi na Mungu akawasikia na kuwasaidia.
Usikubali kuumizwa na maneno mabaya unayotamkiwa au kuyasikia yakisema vibaya juu ya maisha yako mwaamini Mungu yapinge kwa maombi na Mungu atawashangaza watu kwa jinsi atakavyokuinua na kukufanikisha.
jamesmtiba@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.