Heade

MAJERUHI WAWILI WA AJALI YA GARI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI PWANI

Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani wakituhumiwa kuhusika na biashara ya usafirishaji wa bangi .
Majeruhi hao ambao ni Gudlack Kundaeli 24 mkazi wa kiwarani na Ally Gebra maarufu kama Mtena 28 mkazi wa Gongo la mboto wakiwa wote wanatokea  jijini Dar es salaam wanatuhumiwa kukutwa na kilo elf7,mia 500 za bangi katika gari walilokuwa wanasafiria.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amesema watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la Mathias mjini Kibaha baada ya upekuzi uliofanyika kwenye gari aina ya Toyota walilokuwa wakisafiria na kueleza kuwa hayo yaligunguliwa wakati gari hilo lilipopata ajali majira ya usiku.

No comments

Powered by Blogger.