Heade

UNAONA NINI MBELE YAKO?

              

Natumai kuwa unaendelea kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyokulinda na kukutetea katika mambo mengi toka  umeunza mwaka huu wa 2018.
Mpaka sasa kuna mambo mengi yametokea na wengi wamekutwa na mengi na kuwafanya kusononeka na hata kukata tamaa ikiwa bado ni mapema kabisa toka wauanze mwaka.
Napenda kukumbusha kuwa Mungu amekupa uzima na unaendelea kuwa hai kwa sababu ana makusudi na wewe.
Huenda umesahau kutambua kuwa uzima ulio nao ni kwa sababu Mungu ana makusudi na wewe na ndio maana nakukumbusha kwa kukuuliza kuwa unaona nini mbele yako? 
Ukisoma Mithali 29:18 inasema pasipo maono watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Mambo mengi yasiyompendeza Mungu ambayo ni hatari na yana madhara makubwa katika maisha yako unayafanya kwa sababu hauna maono(hauna malengo).
Wakati mwingine umekuwa na bidii, mtafutaji mzuri wa fedha lakini fedha unayoipata hakuna chochote cha maana unachoifanyia imepotea kwa kufanya mambo yasiyokuwa na maana. Umeitumia kuandika heshima baa,mletee yule tano, mwongezee yule tatu, ametumia kiasi gani nimlipie, umekuwa mtoaji mzuri wa zawadi zisizokuwa na umuhimu na mwisho wa siku umejikuta hali yako ya  maisha iko palepale hakuna lolote ambalo familia yako inaweza kujivunia.
Umekuwa mtu wa kuoa kila uchao kwani kila mwanamke unayempata unamfanyia madharau na ukimtishia kuwa fedha unazo na haukawii kutafuta mwingine na kwa sababu mawazo yako umeyaelekeza hivyo kosa kidogo umemfukuza haumtaki tena unaoa mwingine na mwaka ukiisha unakuta umeisha oa zaidi ya mara nne na hauna hata mmoja unapanga kuoa tena januari ya mwaka mwingine, hivyo bidii yako na fedha zote unazozitafuta zinaishia kwenye mahali.
Hii ni kwa sababu hauna maono hivyo unashindwa kujizuia maana ukiwa na maono ya kuwa baba wa familia nzuri na bora utakaye igwa na watu wengine na kuwa kielelezo katika ukoo na jamii yako huwezi kufanya hayo. Unaona nini mbele yako?
Huenda wewe ni mwanafunzi lakini umekuwa wa kwanza kuhimiza migomo na kukwepa baadhi ya vipindi na wakati wenzako wanajisomea wewe uko bwenini unaangalia yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mbaya zaidi ni yale yasiyokuwa na faida yeyote kwako, ukifungua facebook ukitoka unaingia Instagram bado umetenga muda wa twita na haujakutana na marafiki uliowahidi kuwa siku haitapita haujawatafuta kwa WhatsAp.
Wazazi nyumbani wanajua mwanao unasoma na wanatarajia matokeo mazuri katika mitihani yako ya mwisho na kwa sababu wakati unayafanya hayo muda haukukusubiri mitihani inafika huna salio lolote kichwani unacho ambulia ni ziro.Nikuulize tena, unaona nini mbele yako?
Kama ni mtu uliyepanga kusoma na kufanya vizuri ili baadaye wewe mwenyewe na wazazi wako mfurahie pale walipojinyima wakakupa wewe ili uendelee na masomo hutafanya mchezo hata kidogo maana mbele yako umepanga kushinda na kuifanya elimu kuwa moja ya nyenzo mahususi kukutoa mahali ulipo na kukuweka katika nafasi nyingine iliyo nzuri zaidi.
Umekuwa mwanafunzi mzuri wa kuaga nyumbani ninaenda kupata masomo ya ziada tution, ninaenda kujadiliana na wenzangu (group discussion) kumbe unakoenda unajua mwenyewe mwisho wa siku umeleta matokeo mengine nyumbani tofauti kabisa na ya mtihani, tatizo ni kwamba haukua na maono haukulenga kufanya chochote.Unaona nini mbele yako?
Sipedi kukuchosha sana lakini nimalize kwa kukukwambia kwamba kama hauna maona hutaacha kujizuia na hivyo itakuwa rahisi kufanya mambo yatakayokuletea huzuni na sononeko lisilokuwa na ukomo.
Jitahidi sana kuweka maono(malengo) katika muda wa uhai ulionao na uyasimamie maana hayo yatakuzuia kufanya mambo ambayo yako nje na mipango yako na yanayoweza kukufanya uione hii dunia kama si mahali sahihi pa wewe kukaa.
Mungu aufungue ufahamu wako na akupe neema ya kuelewa na hatimaye ubadilike na hata kuwasaidia wengine kubadilika. AMEN
jamesmtiba@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.