FAIDA YA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA BORA
Ili kuwa na afya njema ni muhimu kula vizuri . kula
vizuri si rahisi ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chips, kuku,
au mayai na vingine haya ni mazoea mabovu.
kula vizuri si lazima kula vyakula unavyovipenda bali ni kula vyakula
vyenye afya na kujenga mwili wako. njia moja mbadala ya kuhakikisha unakula
vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula.
FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA.
Kufahamu kirahisi ni vyakula vipi vyenye afya na mahitaji yako mfano mzuri
ni kuwa na uwezo wa kula matunda na vyakula vya protini kwa wingi.
Ni rahisi kujua virubisho muhimu unavyokula kwa kipindi cha wiki nzima
hivyo ni rahisi kukusaidia kutathmini afya yako kwa uraisi.
Kuwa na chaguo zaidi ya moja ya vyakula hivyo na kuzuia kula chakula cha
aina moja kinachopendelewa na kusababisha kukosa virutubisho muhimu kwenye vyakula
vingine.
Kudumisha furaha nyumbani kwa sababu kila mmoja ataona umuhimu wake katika
mawazo juu ya chakula, hivyo kuwafanya watu kufurahia kujumuika kula pamoja
kifamilia.
NB;
Ni vizuri kuwa na ratiba ya chakula kwa wiki nzima hii
itasaidia kujua milo ya chakula kila siku na jumla ya virurubisho unavyopata
mwilini .
Ratiba ya wiki itakusaidia kujua ni kiasi gani cha chakula kinahitajika
mwilini mwako kama uko peke yako au na familia.
JINSI YA KUANDAA RATIBA YA CHAKULA.
Hakikisha unapata vyakula muhimu. Angalia aina za
vyakula kwa siku matunda na mboga mboga hizi ni muhimu kuwepo kwa sababu zina
virutubisho halisi vinavyohitajika mwilini.
Pendelea vyakula halisi (Natural foods). Ni rahisi sana kula vyakula visivyo na virutubisho nyumbani sababu ndivyo
vyakula vilivyojaa kila kona ya dunia kwa sasa.Ili kuwa na afya bora pendelea
zaidi kula vyakula halisi kuliko vile vya kuchakachua, kunywa maji ni muhimu
sana lakini wengi tunapuuzia hii kanuni ya afya mfano mtu mzima anatakiwa
kunywa maji lita moja na nusu kwa siku ingawa wengi wanapendelea kunywa maji
pale wanapohisi kiu tu.
Kuwa mbunifu.
kula ni haki yako lakini kwanini ule chakula cha aina moja wakati kuna
vyakula vingi vya kuijenga afya yako? cha muhimu ni kujifunza kuandaa vyakula
tofautitofauti ,kula vyakula aina mbalimbali ili kuweza kutimiza hili, jaribu
kula vyakula tofauti kutokana na ratiba yako na ni muhimu kutopendelea vyakula
kwenye kundi moja sababu unakosa virutubisho kutoka kwenye makundi mengine.
NB;
UNASHURIWA UWE NA RATIBA YA CHAKULA NYUMBANI NA NI VIZURI KWA AFYA PIA
KWA KUJUA MATUMIZI YA NYUMBANI , ME HUWA
NAFANYA HIVI KILA WAKATI NA NIMEONA FAIDA ZAKE NA NDIO MAANA NAKUSHAURI NA WEWE
KAMA UNAPENDA BASI WASHAURI NA WENZIO KWANI KILA KIZURI NI VIZURI KUWAELEZA NA
WENZIO. BY levyzevoice@.com ,mobile
phone:0759820684
No comments