BARAZA LA CHUO KIKUU UDOM LIMEPITISHA SERA YA HAKI MILIKI ZA KITAALUMA
Baraza la chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) limepitisha sera ya haki miliki za
kitaaluma ikiwa ni njia inayolenga kuwabana wezi wa kazi za kitaaluma ,
kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa kutoa uhakika wa haki za watafiti.
Akizungumza katika mahafali ya 8 ya chuo hicho mwenyekiti wa baraza hilo
Gaudensia Kabaka amesema sera hiyo itasaidia kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa
kutoa haki za watafiti,wanafunzi na wahisani.
Aaidha Kabaka amesema kupitishwa kwa mpango huo ni kukipandisha hadhi kituo
cha afya cha Chuo hicho kuwa hospitali na utaratibu umeanza kuhakikisha azma
hiyo inafikiwa.
No comments