Heade

SADAKA INA NGUVU KUBWA YA KUFUNGUA YALIYOFUNGWA KWA MUDA MREFU


Namshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa uhai heshima na utukufu apewe BWANA pia ni matumaini yangu makubwa kuwa unaendelea kuyafuatilia masomo haya na Mungu anazidi kukuwezesha kwa neema yake kuendelea vema katika shughuli zako za kila siku .
Sadaka ina nguvu kubwa ya kuyafungua yaliyofungwa kwa muda mrefu. Ni kweli kwamba kwa sehemu kubwa maombi ndiyo silaha ya kuleta ushindi na kuwatoa watu kwenye vifungo vya ibilisi lakini leo napenda kukumbusha kuwa sadaka ina nguvu kubwa ya kuyafungua yaliyofungwa kwa muda mrefu.
Unaweza kuwa umekaa katika ndoa kwa muda mrefu na haujapata mtoto pamoja na kwamba umefanya jitihada za kila namna ikiwa ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi hospitali mbalimbali kubwa ndani na nje ya nchi, pengine unao ugonjwa fulani na umetibiwa siku nyingi katika hospitali mashuhuri lakini haujapata kupona au umejaribu kufanya biashara na kutumia mtaji mkubwa lakini umekuwa mtu wa kuanguka mtaji na kufilisika kila uchao nikwambie  kuwa tatizo hilo linaweza kufunguliwa kwa sadaka na historia yako ikabadilika.
Ukisoma biblia katika kitabu cha 2Wafalme 4: 8 -17 utaona habari za mwanamke mmoja wa huko Shunemu, anatoa sadaka yake kwa kumtumza mtumishi wa Mungu Elisha kwa kumpa chakula na kumwomba mmewe kukubali kumjengea chumba kidogo cha kupumzika mara apitapo nyumbani mwao.
Na baada ya mume wake kukubali kufanya hivyo ,mtumishi wa Mungu kila alipo pita katika njia hiyo, alipita kwao kula chakula na kupumzika  katika chumba hicho.
Siku mtumishi wa Mungu alipotaka kuondoka alimwita mwanamke na kumwambia, tazama umetundea wema kiasi hiki utendewe nini basi?
Mwanamke huyu hakuweza kuomba kitu chochote kwa wakati huo, lakini Gehazi mtumishi wa mtumishi wa Mungu Elisha akamwambia Elisha hakika hana mwana na mume wake ni mzee. Kumbe mwanamke huyu hakuwa na mwana hadi anafikia uzee kwa maneno mengine alikuwa tasa.
Mtumishi wa Mungu Elisha akamtabiria kupata kuzaa na kweli akazaa mtoto. 
2Wafalme 4:8-17 neno la MUNGU linasema;Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu;na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo;naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile huingia kula chakula. Yule mwanamke akamwambia mumewe, tazama mimi naona kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.
Nakuomba tumfanyie chumba kidogo ukutani na ndani yake tumwekee kitanda,na meza , na kiti na kinara cha taa, na itakua, atujiapo, ataingia humo.
Ikiwa siku moja akafika huko akaingia katika chumba kile akalala. Akamwambia Gehaza mtumishi wake, mwite yule mshunami.Naye alipokwisha kuitwa ,akasimama mbele yake. Akamwambia, sema naye sasa .Tazama wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi?Je uombewe neno kwa mfalme au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu ,mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe. Akasema basi utendewe nini?Gehazi akajibu, hakika hana mwana na mumewe ni mzee. Akamwambia kamwite na alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. Akasema panapo ,wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema la! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu,usiniambie mimi mjakazi wako uongo.Yule mwanamke akachukua mimba,akazaa mtoto mume wakati uo huo mwakani kama Elisha alivyo mwambia.
 Mpenzi msomaji wangu kilicholifungua tumbo la mwanamke  huyu aliyekaa muda mrefu bila kupata mtoto ni sadaka ya kumtunza mtumishi wa Mungu Elisha kwa kumlisha chakula na kimjengea chumba cha kupumzika.
Maana kama asingelimkaribisha kwa kumshurutisha aje ale chakula na baadae kumwomba mumewe wamfanyie chumba kidogo, asingeweza kuonana naye na asingejua kama hana mwana. Rafiki yangu na msomaji wangu katika BWANA, sadaka yako utakayoitoa kwa moyo kwa ajili ya kazi ya Mungu na kuwalisha au kuwatumza watumishi wa Mungu itakuondolea matatizo na changamoto zilizoshindakana kwa muda mrefu.
Mungu akusaidie unapo usoma ujumbe huu, fahamu zako pamoja na moyo wako vifunguliwe katika eneo la utoaji ili uwe miongoni mwa watu waliopiganiwa na sadaka zao na nguvu ya kuyashinda matatizo, changamoto na vikwazo vinavyozuia Baraka za Mungu kwako iambatane nawe na kukushindia kwa jambo lolote na wakati wote AMINA.
jamesmtiba@gmail.com                                                           

No comments

Powered by Blogger.