Heade

MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU

Najua unatamani kuona yale uliyoyapanga kuyafanikisha katika mipango yako ya maisha hapa duniani yanakamilika kulingana na uhitaji wako lakini mara nyingi umeumiza kichwa kwa mawazo na maswali mengi ni kwa nini umekuwa katika hali ya kuchelewa.
 Ukitathimini zaidi unaona wakati unawaza kufanya miongoni mwa mambo uliyoyapanga uliona kuna mpenyo na  nafasi kubwa ya kutimiza malengo yako ila toka uamue kuanza, umeshangaa kuona hakuna mlango wowote wa kuingilia katika kuyatimiza malengo hayo.
Na hivyo muda mwingi umepita,miaka imezidi kukatika umri nao unakwenda mbio na hii imekupa wasiwasi hata msongo wa mawazo pia limekuwa jambo linalokufanya ujisikie kuvunjika moyo na kukata tamaa.
Usikate tamaa tambua kwamba wapo watu unao waona wakiwa na mafanikio makubwa lakini kabla ya kuwa kama walivyo walipitia mambo mengi sana na magumu mno ikiwemo kuchelewa kupata yale waliyoyahitaji lakini kwa kuvumilia kwao leo hii wameyasahau makovu na maumivu ya kuchelewa kuyapa waliyoyatamani kwa muda mrefu.
Ukisoma biblia katika kitabu cha mwanzo 21:1-7 utaziona habari za Ibrahimu na Sara ambao walikaa muda mrefu bila kupata mtoto suala lililowafanya wabakie katika kiu kuu ya kupata mtoto lakini miaka ilizidi kusongea bila kuwa na mtoto hawakukata tamaa waliendele kumwamini, kumwomba na kumtolea Mungu sadaka na katika kuvumilia kwao Mungu akawapa Isaka mtoto wa pekee katika siku za uzee wao na maisha yao yakabadilika kabisa Ibrahimu ambaye hakuwa na mwana kwa muda mrefu,anapata mtoto akiwa na umri wa miaka mia na Mungu anamfanya kuwa baba wa mataifa,hakika unaweza kuona hili si jambo la kawaida kusubiri kwa kipindi cha miaka mia moja ni muda mrefu sana na hapa ndipo unaweza kujiuliza, kwa nini unawaza kukata tamaa mapema?mimi nikwambie kuwa changamoto yako haijamshinda   MUNGU isipokuwa unaweza kupoteza muujiza wako kwa kukata tamaa na kukosa mambo mazuri anayokuwaziwa BWANA kama anavyosema katika kitabu cha Yeremia 29 :11
Na hivyo nikwambie pamoja na hilo jambo unaloliona kuwa ni mtihani mgumu kwako si kitu mbele za BWANA usikubali kukata tamaa tambua katika kuchelewa kwako kuna ushindi mkubwa mbele.
Endelea kufuatilia jumbe hizi na Roho Mtakatifu aliye mwalimu wa kweli akuwezeshe kuelewa na hatimaye uishinde hali ya udhaifu uwe na moyo mkuu.

0766020002

No comments

Powered by Blogger.