Heade

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YATOA MIKOPO

Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu HESLB imetoa mikopo kwa wanafunzi elfu kumi na mia moja tisini na sita wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018 katika awamu ya kwanza.
Mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo Abdul Razaq Badru amesema jumla ya shilingi bilioni 34.6 zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao ameongeza kuwa bilioni 108.8 zitatolewa kwa  wanafuzi elf 30,000 wa mwaka wa kwanza   wa masomo 2017/2018.
Aidha amewakumbusha wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wanasifa zakupata mikopo watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kudhibitisha chuo watakacho jiunga kwaajili ya masomo.

Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa katika mwaka wa masomo wa 2017/2018 bodi imetenga shilingi bilioni 318.6 kwaajili ya wanafunzi wanaoendelea na masomo na tayari fedha hizo zimeanza kutumwa kwa wanafunzi wanaendelea na masomo.  

No comments

Powered by Blogger.