BENKI NA TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUTOA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA WA CHINI NA WA KATI.
WAZIRI wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezitaka benki na taasisi za
fedha nchini kuanza kuweka mikakati ya makusudi ya kushirikiana na serikali
katika kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda
Akizungumza
katika maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa benki ya Afrika BOA tawi la
Tanzania jijini Dar es salaam amesema ni vema taasisi za fedha na mabenki
yakaanza kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa chini na wa kati ili kuwawezesha
kuanzisha viwanda vya kati hiyo badala ya kushughulika na wafanyabiashara
wakubwa ambao ni wachache.
Aidha waziri Mwijage amesema serikali ina mkakati
wa kuangalia upya mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili kuboresha zaidi
mazingira hayo kwa lengo la kuondoa urasimu na kuvutia uwekezaji zaidi nchini
huku akiipongeza Benki ya Afrika kwa kutoa huduma nzuri kwa watanzania suala
ambalo limechochea kuinua hali ya maisha ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Naye mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ammish
Owusu Amoah amesema benki hiyo imefanikiwa kuwa benki ya kipekee na mfano
katika uwepo wake nchini kutokana na kutoa huduma za kipekee na kwa asilimia
100 ukilinganisha na benki nyingine ambazo zinafikia asilimia kati ya 70 na 80
ya utoaji wa huduma.
No comments