MIMBA ZA UTOTONI BADO NI TISHIO MKOANI KATAVI
Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenerali Msataafu Raphael
Muhaga amesema kuwa mimba za utotoni bado ni tishio kubwa katika manispaa ya
mpanda mkoani Katavi ambako wasichana 624 walio na umri chini ya miaka 18
wamejifungua katika vituo vya afya vilivyopo katika manispaa hiyo.
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia mkoani humo katika viwanja vya sabasaba kabungu wilayani
tanganyika.
Meja jenerali Muhaga amesema kuwa taarifa kutoka katika
vituo vya afya vya manispaa ya mpanda ya kipindi cha mwaka jana inaonyesha
wasichana 624 walijifungua kiwango ambacho ni
tishio katika mkoa wa katavi.
Aidha kuhusu unyanyasi wa kijinsia amesema kuwa kesi
1,178 zimeripotiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo na
maofisa ustawi wa jamii mwaka 2016.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa katavi Damas
Nyanda amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali kwa kushirikiana
na makundi mbalimbali ya kijamii takwimu bado zinaonyesha ongezeko la ukatili
wa kijinsia kuwa kubwa.
No comments