Heade

MAZUNGUMZO YA KUUNDA SERIKALI YA MUUNGANO UJERUMANI BADO UTATA

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema kuwa vyama vinavyoshiriki katika mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano vya CDU/CSU na chama cha SPD bado vinakumbwa na vizingiti vinavyohitaji kuondolewa kabla ya kufikia makubaliano ya kuunza mazungumzo rasmi.
 Akizungumza leo ambayo ni siku ya mwisho ya mazungumzo ya awali, Merkel amesema itakuwa siku ngumu, lakini atashiriki kwa uwezo wake wote akitambua wazi kuwa Wajerumani wanatarajia matokeo. Miezi mitatu tangu ulipofanyika uchaguzi wa Ujerumani,
 Merkel ambaye amedhoofishwa anategemea matokeo mema ya mazungumzo hayo na SPD ya kuunda serikali ya muungano ili kuhudumu kama kansela kwa muhula wa nne. Muungano huo wa vyama vikubwa umeitawala Ujerumani kati ya 2013 hadi 2017.

No comments

Powered by Blogger.