Heade

MJADALA WA KUMSHTAKI JACOB ZUMA WAENDELEA

 


 Kamati ya Kudumu ya Kanuni za Bunge inakutana leo Jumanne kukamilisha masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa kumshtaki bungeni na kumwondoa rais.

Awali kamati hiyo ilikutana Alhamisi iliyopita kujadili pendekezo la “jopo mchanganyiko” lenye wabunge, majaji wastaafu na wanasheria watakaoweza kushughulikia kwa kina mchakato wa kumshtaki rais.

Mchakato huu ndio unapewa uwezekano wa kutumika dhidi ya Rais Jacob Zuma, endapo atapuuza wito wa kumtaka ajiuzulu. Kilichosalia ni kukamilisha mchanganyiko wa watu katika kamati au jopo na mchakato wake kabla ya kuwasilisha ripoti kwenye kamati ya pamoja ya kanuni kisha kuisoma ndani ya Bunge la Taifa.

"Kuna uamuzi wa namna mbili ambao unaweza kujadiliwa na kamati ya kanuni,” mwenyekiti wa kamati ndogo Richard Mdakane aliliambia shirika la News24.

"Upande mmoja ni kuwa na uwakilishi unaofanana wa wabunge; kwamba kila chama kitateua mwakilishi mmoja. Upande wa pili ni kuwa na uwakilishi wenye uwiano. Kamati zote za Bunge zinawakilishwa kwa uwiano na vyama vidogo vitahudhuria kamati zote."

Mdakane amesema chama cha ANC kimekutana kupitia jopo la ufundi na kinaamini jopo lazima lizingatie uwiano jumuishi, lakini ni juu ya kamati kujadili.


No comments

Powered by Blogger.