Heade

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YATIBU WATU 64,063

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ni tegemeo kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na inayoshika nafasi ya tatu kwa utoaji huduma za magonjwa ya moyo, kwa mwaka wa 2017 imeona jumla ya wagonjwa 64,093 kati yao wa nje wakiwa 60,796 na waliolazwa 3,297.
Aidha, Serikali imeokoa zaidi ya Sh bilioni 29 ambazo ingezilipa kwa kupeleka nje wagonjwa 1,025 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua nchini. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.
Hayo yamo katika taarifa ya taasisi hiyo kwa umma, ikielezea mafanikio yake katika mwaka uliopita. Imesema wagonjwa 30,10 waliolazwa waliruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri na wagonjwa 287 walipoteza maisha hii ikiwa ni sawa na asilimia 8.7.
Imesema wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa 25 walifariki dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13).
Kati ya wagonjwa 225 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 60 na watu wazima 45.
Taarifa hiyo imesema upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 800 kati ya hao 798 wanaendelea vizuri na wagonjwa wawili (2) walifariki ikiwa ni chini ya asilimia 1.6.
Kati ya wagonjwa 800 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 631 walifanyiwa upasuaji na madaktari wa ndani. “Tulikuwa na jumla ya kambi za matibabu 15. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika.
Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 80 na watu wazima ni 40. Wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 92 na watu wazima 77.
“Tulifanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVFArterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafi shia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya fi go (Hemodialysis) 52,” imeeleza zaidi sehemu ya taarifa hiyo.
Wakati huo huo, taasisi hiyo imesema ilishiriki katika utoaji wa huduma ya upimaji afya bila malipo na kutoa elimu ya afya bora ya moyo kwa wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Lindi na Katavi.

No comments

Powered by Blogger.