Heade

WANANCHI WA WILAYA YA TARIME MKOANI MARA WAOMBWA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Tarime Bw Mkaruka Kura amewaomba wananchi kuungana kwa pamoja kuibadilisha wilaya ya Tarime kwa kuiletea maendeleo.

Bw Mkaruka ameyasema hayo wakati wa kumpokea mwanachama mpya bw Nyirabu Kitunga Nyirabu baada ya kuamua kuhama chama cha ACT wazalendo na kuhamia CCM.

Mkaruka amesema kuhama chama kimoja kwenda kingine ni utashi wa mtu na wanachi kuondoa dhana potofu kuwa wanaohama chama kimoja kwenda kingine wamenunuliwa au kushawishiwa.

Aidha Bw Nyirabu Kitunga aliwahi kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Kitale mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha ACT wazalendo na hatimaye kushindwa na Leonard Kasuku ambaye ndiye diwani wa kata hiyo kwa sasa.

Hatahivyo Nyirabu amesema kuhamia CCM ni uamuzi wake na ushawishi mkubwa kutoka kwa mh rais dk Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya.

No comments

Powered by Blogger.