Heade

HAKIKA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AANZA KUBADILIKA



WaandamanajiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKulikuwa na maandamano mjini Washington dhidi ya uamuzi wa Trump
Serikali ya Rais Donald Trump imeongeza kinga ya muda kwa karibu wakimbizi 7,000 wa Syria wanaoishi nchini Marekani wakati vita vikiendelea nchini mwao.
Walikuwa wamepewa kinga ya muda dhidi ya ya kurejeshwa nyumbani chini ya mpango wa kibinadamu unaofahamika kama -Temporary Protected Status (TPS).
Rais Trump amefuta mpango huo kwa nchi mbali mbali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, na hivyo kuwaathiri wahamiaji kutoka kutoka El Salvador, Haiti na Nicaragua.
Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen M Nielsen
Image captionWaziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen M Nielsen anasema kuwa Marekani itachunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika
Marekani ilisema kuwa haitakubali maombi ya wahamiaji kupitia TPS kutoka Syria.
"Ni wazi kwamba hali iliyoyopelekea Syria kuchaguliwa ina msingi wa kuendelea kuwepo, kwa hivyo kurefushwa kwa muda wa kinga kwa wakimbizi kunakubalika chini ya sheri ," alisema waziri usalama wa ndani Kirstjen M Nielsen katika taarifa yake.
"Tutaendelea kuchunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika. Kwa raia wa Syria ambao tayari wanaishi na kufanyia kazi nchini Marekani, mpango wa TPS utarefushwa kwa miezi mingine 18. Lakini Wasyria walioingia nchini Marekani baada ya Agosti 2016 watatengwa na mpango huo licha ya kuendelea kwa hali mbaya nyumbani."
Mpango wa hadhi ya ulinzi kwa raia wa Syria ulipangwa kufikia kikomo tarehe 31 Machi.
Mapema mwaka huu, Wizara ya Usalama wa Ndani ilitangaza kuwa itafikisha kikomo mpango wa kinga kwa raia 262,500 kutoka El Salvador, ingawa hatua hiyo itacheleweshwa kwa miezi 18.
Mwezi Novemba, utawala huo ulisema kuwa hadhi ya ukimbizi ya raia takriban 59,000 wa Haiti itakwisha 2019.

No comments

Powered by Blogger.