Heade

JUKWAA LA VIJANA NA KANISA


Ni mkutaniko wa vijana unaowaweka vijana pamoja na kuwapa fursa ya kujadili changamoto na mambo mbalimbali yanayowaweka vijana mbali na Mungu , yanayowafanya vijana washindwe kuishi maisha ya kumcha Mungu.

Katika kipindi cha redio kilichorushwa kupitia Redio Sachita 88.1 Tarime Mara Tanzani, ambapo vijana walikaa pamoja kujadili mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kijana kuwa na baba wa kiroho , changamoto zinazowakwamisha vijana kuishi maisha ya kumcha Mungu na jinsi ya kuziepuka pamoja na nafasi ya familia kumwezesha kijana kuishi maisha ya kumlingana Mungu haya yalibainiwa.

BAADHI YA MAMBO NA CHANGAMOTO ZINAZOMFANYA KIJANA AKAE MBALI NA MUNGU.
Kutothaminiwa katika nyumba za ibada, vijana wengi wanarudi nyuma na hata kukata tamaa ya kuendelea kushiriki ibada kwa kuto oneshwa kuwa wana thamani na ni watu muhimu katika nyumba za ibada na masuala mbalimbali yanayoendeshwa katika nyumba za ibada.

Mara nyingi vijana wenye vipawa na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuimba, kupiga vyombo vya muziki na kutoa mahubiri wanapohitaji kufanya hivyo na kunyimwa nafasi hujisikia vibaya na hatimae hukata tamaa na kuchukua maamuzi ya kuchagua kufanya mambo mengine nje ya nyumba za ibada ambayo mengine huhamisha na kuharibu kabisa mwenendo na tabia njema waliyokuwa nayo vijana hao.

Aina ya makuzi waliyoyapata toka utotoni; Kwa sehemu kubwa mwenendo  mwema au mbaya kwa kijana huchangiwa na aina ya makuzi au malezi aliyoyapata kijana toka utotoni, kama wazazi walimfundisha na kumwendeleza kumcha Mungu ni rahisi sana kuweza kujisimamia mwenyewe katika kumcha Mungu.

Lakini kama wazazi hawakumwandaa kijana mapema kuishi maisha ya kumcha Mungu ni vigumu sana kubadilika pale anapokuwa katika umri mkubwa vinginevyo nguvu kubwa itahitajika kumbadilisha.

Mfano,kama wakati wazazi wanaenda ibada wana waacha watoto nyumbani na wakati mwingine kuwapangia majukumu kama vile kufanya usafi wa nguo zao, kufagia uwanja na hata kuwambia mkimaliza mkacheze kwa akina Fulani ,watoto hawa wakiwa wakubwa na kufikia umri wa ujana hawatakuwa na uelewa  wowote juu ya umuhimu wa kumfanyia Mungu ibada.

Migogoro ndani ya nyumba za ibada;kuna baadhi ya nyumba za ibada zimebaki kuwa sehemu ya marumbano yasiyokuwa na ukomo na hata kupigana vijembe kila uchao hali hii huwafanya vijana wengi washindwe kutofautisha mahali anapo abudiwa Mungu na maeneo mengine kama vijiwe vya masengenyo vinavyopatikana kwa baadhi ya mitaa.
Migogoro hii ambayo mingi huchochewa na makundi ndani ya nyumba za ibada ambayo huwa na malengo kinzani hili linamtaka Fulani kuwa kiongozi au mchungaji/askofu na jingine linasema huyu hafai mambo haya yamewafanya vijana wengi kukata tamaa na kukaa mbali na nyumba za ibada.

Kuhudumia watu kwa makundi katika nyumba zetu za ibada; kuna baadhi ya nyumba za ibada huwatenga watu na si kwa kitu kingine ila uwezo wa kiuchumi, utakuta viti vime andaliwa kwa ajili ya watu Fulani haijalishi anamcha Mungu kwa kiwango gani lakini kwa sababu ana uwezo kiuchumi hata mwanzo au mwishoni mwa ibada utasikia kiongozi wa ibada siku hiyo anatoa shukrani kubwa na kumsifu,nakushukuru sana Bwana Fulani kwa kuwa pamoja nasi, wewe ni mtu muhimu tunakutegemea na kuongea mengine mengi tu hivi vyote ni miongoni mwa mambo yanayowakosesha vijana ari ya kuendelea kuona umuhimu wa kumcha Mungu.

 UMUHIMU WA KIJANA KUWA NA BABA WA KIROHO

Mchungaji Peter Endrew anasema mtu kuitwa baba wa kiroho si jambo jepesi kama watu wanavyoweza kufikilia kwa sababu kuna kazi kubwa kwa huyu baba wa kiroho na si kila mtu anaweza kuwa baba wa kiroho na kumwita mtu baba si suala dogo.

Hii yote ni kwa sababu ya majukumu makubwa na mazito anayokuwa nayo baba wa kiroho ikiwa ni pamoja na kufuatilia mwenendo wa kijana na kuwa mshauri wake wa mara kwa mara kuhakikisha kuwa kijana anaendelea kuishi maisha ya kumcha Mungu, suala ambalo si rahisi sana kama linavyotamkika.

Lazima awe mtu wa kuelewa changamoto na matatizo mbalimbali yanayomkumba kijana katika maeneo yote. 

No comments

Powered by Blogger.