Heade

KIONGOZI MWINGINE WA UPINZANI AKAMATWA KENYA


Mbunge wa makadara George Aladwa ni mwanasiasa wa tatau wa upinzani kukamtwa na maafisa wa polisi tangu kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipojiapishaHaki miliki ya pi
Image captionMbunge wa makadara George Aladwa ni mwanasiasa wa tatau wa upinzani kukamtwa na maafisa wa polisi tangu kiongozi wa upinzani Raila Odinga alipojiapisha
Mbunge mwingine nchini Kenya, amekamatwa kuhusiana na mzozo unaozunguka kujiapisha kwa aliyekuwa waziri mkuu Raia Odinga kwa kile anachokitaja kama rais wa watu wa Kenya.
Mbunge wa Makadara jijini Nairobi George Aladwa alikamatwa asubuhi ya Jumamosi nyumbani kwake na maafisa wa idara ya upelelezi na kupelekwa hadi makao makuu ya idara hiyo kwa mahojiano zaidi.
Aladwa ambaye amewahi kuwa meya wa jiji la Nairobi, alikuwa katika mstari wa mbele katika mipango ya sherehe hizo ambayo haikuwa na idhini ya serikali.
Aladwa sasa ni mbunge wa pili kukamatwa kuhusiana na hafla hiyo ambayo pia imeshutumiwa na jamii ya kimataifa.
Mbunge mwingine wa Nairobi Tom Kajwang alikamatwa na kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana.
Mwanaharakati mwingine wa upinzani wakili Miguna miguna pia alikamatwa siku ya Ijumaa na angali anazuliwa na polisi licha ya mahakama kuruhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kula kiapo cha 'kuwa rais wa watu'Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kula kiapo cha 'kuwa rais wa watu'
Bwana Aladwa alikamatwa siku ya Ijumaa usiku katika nyumba yake iliopo Buruburu kulingana na kiranja wa walio wachache bungeni Junet Mohamed.
Bwana Mohammed ambaye pia mbunge wa Suna Mashariki alisema kuwa bwana Aladwa kwa sasa anazuiliwa katika makao makuu ya ujasusi.
Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kukamatwa kwa Aladwa.

No comments

Powered by Blogger.