Heade

MWINJILISTI GRAHAM AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 99


Billy GrahamHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa alikuwa amehubiria jumla ya watu milioni 210
Mhubiri wa injili Billy Graham, aliyepata umaarufu mkubwa duniani katika karne ya 20 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Graham, raia wa Marekani, alieanzia kuhubiri jijini London Uingereza mnamo mwaka 1954, alikusanya maelfu ya watu kila mahali alipofanya mikutano ya hadhara ya injili.
Afrika Mashariki, Graham aliwahi kuhubiri Tanzania, miaka 55 iliyopita, wakati nchi iliitwa Tanganyika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika miaka ya 1960. Takriban "watu 40,000 walihudhuria mkutano huo wa siku moja, tarehe Feb 28. 1960", kwa mujibu wa mtandao wa shirika lake.
Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa amehubiri kwa jumla ya watu milioni 210.
Alikuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kuanza huduma ya mahubiri mwaka 1939.
Image captionWakati akifuzu Billy tayari alikuwa amepata wito wa injili
Graham, ambaye alifanya kazi kama afisa wa mauzo, aliendelea na kuwa mmoja wa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa watu wa dini zote huku akiwashauri marais na viongozi wengine wengi duniani juu ya imani ya Kikristo.
Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles.
Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kuwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Image captionGraham(kulia) akiwa ni msimamizi wake wa muziki Cliff Barrows
Ni muhubiri aliyeepuka kashfa mbalimbali zilizowazonga wahubiri wengi waliotumia runinga kusambaza injili.
Alijenga uhusiano wa kirafiki na marais kadhaa wa Marekani kuanziaTruman hadi Nixon na hata Obama. Mkutano wake wa mwisho wa hadhara ulikuwa mwaka 2005 jijini New York Marekani akiwa na umri wa miaka 86.
Rais Donald Trump amemuelezea Graham kama "mwanaume wa kipekee".
Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema "Mhubiri maarufu wa Injili Billy Graham. Hakuna aliyekuwa kama yeye! Atakumbukwa na Wakristo na watu wa dini zote. Mwanamume wa kipekee kabisa."

No comments

Powered by Blogger.