MGANGA AKAMATWA KWA KUSABABISHA MAUAJI TABORA
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora SACP Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa za kukamatwa kwa Mganga wa Jadi anayepiga ramli chonganishi na kusababisha Mauaji.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kumkamata mganga wa Jadi mwenye kupiga ramli chonganishi na kusababisha Mauaji ya mama mmoja aliyefahamika kwa jina la NDILU MBOGOSHI, Miaka 65, Msukuma, Mkulima, Mkazi wa Shilabela Kata ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora, ambaye aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani.
Mara baada ya tukio hilo upelelezi ulifanyika na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora liliweza kubaini na kumkamata mganga wa jadi huyo ambaye amefahamika kwa jina la THERESIA PAULO, 57YRS, MSUKUMA, mganga wa jadi na mkazi wa ISAGEGE-SASU Tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua.

No comments