WAKIMBIZI 57000 WAKIMBILIA UGANDA
Idadi ya wakimbizi wa mwaka huu inapita wakimbizi 44,000 ambao walifanya safari kama hiyo katika kipindi cha mwaka 2017 kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Babar Baloch, Wakimbizi wamekuwa wakiingia nchini Uganda kupitia ziwa Albert na kuhatarisha maisha yao mara kadhaa.
Mapigano jimboni Ituri yamehusisha jamii ya Hema na Lendu ambao ni wakulima na wafugaji wenye historia ndefu tangu kuanza kwa uhasama wakigombania ardhi kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.
No comments