Heade

SERIKALI YAWARUDISHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA


Serikali imeagiza watumishi wa umma 1,370 walioajiriwa kabla ya Mei 20, 2004 ambao hawakufaulu mtihani wa kidato cha nne (darasa la saba) na waliondolewa kazini kwa kigezo cha vyeti vya kidato cha nne, warudishwe kazini mara moja, wapewe stahiki zao zote ikiwemo mishahara yao  tangu walipoachishwa kazi.

Hayo ameyasema leo Aprili 9, 2018 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, George Mkuchika, Bungeni Mjini Dodoma na kueleza kwamba, watumishi hao waendelee kubaki kazini mpaka watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.

Aidha, serikali imesema watumishi ambao hawana vyeti vya kidato cha nne na waliajiriwa baada ya Mei 20, 2004, hawatarudishwa kazini.

No comments

Powered by Blogger.