Heade

WATU WATATU WAFARIKI KATIKA MILIPUKO MIWILI

Milipuko miwili ya mabomu imesabaisha vifo vya watu takriban watatu katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Kwa mujibu wa habari,mlipuko mmoja wa gari umetokea katika eneo la usalama na kusababisha kifo cha mtu mmoja na askari watatu.

Mlipuko mwingine umetokea mtaa wa KM5 na kusababisha kifo cha askari mmoja pamoja na mashambuliaji mwenyewe.

Mlipuko wa pili nao ulikuwa ni wa gari ukifuatiwa na urushaji risasi kati ya askari na mshambuliaji.

Hakuna kundi lolote la kigaidi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

No comments

Powered by Blogger.