Heade

MTOTO ASIMAMA KUMUELEZA RAIS MAGUFULI SHIDA ZAO,APEWA MILIONI 3

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mapema leo amemkabidhi mwanafunzi wa kidato cha kwanza Nundoka Msangi, kiasi cha shilingi milioni 3, kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya Sekondari Mangula mkoani Morogoro.

Tukio hilo limefanyika wilayani Mikumi mkoani Morogoro, ambapo Rais Magufuli alisimama katika kijiji cha Mangula kwaajili ya kuongea na wananchi waliokuwa wamesimama wakati wa msafara wake akielekea Wilayani Kilombero.

Baada ya kutoa hotuba fupi, Rais Magufuli aliuliza endapo shule ya sekondari katika eneo hilo ina changamoto yoyote, ndipo kijana Nundoka akajitokeza na kusema hawana vyoo na Rais akachangia milioni tatu na kuwataka wanacnhi kushiriki katika ujenzi wa vyoo hivyo.

''Namkabidhi hii pesa kijana Msangi, naomba zitumike vizuri kwenye ujenzi wa vyoo na niwaombe tu wananchi mshiriki vizuri kujenga vyoo hivyo, nitarudi tena kukagua,'' amesema Rais Magufuli wakati akikabidhi fedha hizo.

Magufuli yupo Mkoani Morogoro akiendelea na ziara yake ya siku tatu ambayo inahusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Baadae leo atazindua daraja la Mto Kilombero Mkoani humo.

No comments

Powered by Blogger.