WADAU WAMPONGEZA SPIKA WA BUNGE MHE.JOB NDUGAI
Wadau wamempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kwa kuonesha nguvu ya Bunge katika kusimamia maslahi ya Taifa, nakubainisha hatua hiyo itaweza kujenga imani kwa wananchi juu ya Bunge lao.
Akizungumza kwenye kipindi cha Easta afrika BreakFast kinachorushwa na East Afrika Radio, mtaalamu wa siasa za kikanda, Amini Mgeni amesema Spika wa bunge la Tanzania amesimamia haki na kuonesha wajibu wa wabunge katika kusimamia maslahi ya wananchi, jambo ambalo linapaswa kuigwa na wabunge wote.
"Hivi ndivyo bunge linavyopaswa kuwa ni mhimili unaojitegemea na unapaswa kuikosoa serikali nakutetea wananchi maana wao ni wakilishi wa watanzania wengi waliowapa dhamana, Spika Ndugai ataheshimika daima kama ataendelea na msimamo wake huu bila kuangalia chama", amesema Amini.
Mei 8, 2018 Spika Ndugai aliyakataa maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage nakumtaka atoe majibu yakueleweka kuhusu uhaba wa mafuta nchini, jambo ambalo Waziri Mwijage aliahidi atalitolea ufafanuzi saa 11 jioni ya siku hiyo hata hivyo ilishindikana na hatimaye jana Mei 9, 2018 akaweza kutolea ufafanuzi.
Msimamo wa Spika uliwakosha pia baadhi ya wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe ambaye aliweza kuelezea hisia zake na kumtaka Spika Ndugai aendelee kuwa kiongozi imara wa bunge kwa kuikosoa serikali pale inapoenda kinyume na maslahi ya wananchi.
No comments