CHINA YAFUNGUA MKUTANO UNAOHUDHURIWA NA URUSI,IRAN, ,,MAREKANI YAJITOA
China leo (09.06.2018) imefungua mkutano wa siku mbili wa usalama wa kanda unaohudhuriwa na Urusi, Iran na washirika wengine, kutokana na Marekani kujitoa katika makubaliano ya kinyuklia na Iran.
Magari ya deraya yamejipanga mitaani katika mji wa pwani wa Qingdao wakati viongozi wa dunia wakiwasili siku ya Ijumaa kwa ajili ya mkutano huo wa 18 wa kila mwaka wa shirika la ushirikiano la Shanghai (SCO), kundi la kimkoa la usalama linaloongozwa na China na Urusi. Mataifa wanachama ni pamoja na Jamhuri nne za iliyokuwa Umoja wa Kisovieti katikati ya bara la Asia , Pakistan na India. Iran ni mwanachama mwangalizi.
Maafisa wamewaondoa watu wote katika eneo la ufukwe la mji huo, wakiwaondoa watu wanaofanya manunuzi , wakaazi na watu wanaotembelea eneo hilo kuwezesha rais wa China Xi Jinping , mwenzake wa Urusi Vladimir Putin na rais wa Iran Hassan Rouhani kupita.
Rais wa Pakistan Mamnoon Hussain na waziri mkuu wa India Narendra Modi pia watahudhuria mkutano huo.
Mkutano huo wa SCO unakuja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa nchi hiyo katika njia ya utata kutoka katika mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 na Iran ambao unaweka ukomo wa mpango wake wa kinyuklia ili kuweza kulegezwa vikwazo vya kiuchumi.
Licha ya kwamba suala hilo halimo katika agenda rasmi , wachambuzi wanasema kwamba mada muhimu ya majadiliano mwaka huu huenda ikalenga juu ya iwapo Iran itaruhusiwa kutoka katika nafasi yake kama mwangalizi wa mkutano huo wa SCO na kuwa mwanachama kamili, hatua ya maendeleo ambayo inaiwania tangu mwaka 2008 lakini imeshindwa kufanikisha kwa sababu ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Makubaliano ya kinyuklia ya mwaka 2015 yameondoa kizingiti hicho.
Hivi sasa kutokana na kujiondoa Marekani kutoka katika mkataba huo, "Wanachama wa SCO huenda wakatumia fursa hiyo kuipa Iran uanachama kama njia ya kuonesha kuiunga mkono pamoja na makubaliano hayo ya kinyuklia," amesema dawn Murphy , profesa wa mitaala ya usalama wa kimataifa katika chuo cha Marekani cha vita vya angani.
Wasiwasi kuhusiana na Iran unakuja wakati suala lingine la kinyuklia linajitokeza , ambapo Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un wanajitayarisha kwa ajili ya mkutano mjini Singapore.
Masuala ya biashara, uwekezaji na ushirikiano wa maendeleo pia yatakuwa mada muhimu katika mkutano huo wa SCO, Murphy amesema , kutokana na hali ya hewa ya "ongezeko la kupambana na utandawazi na mbinyo katika taasisi za dunia za uchumi wa mataifa", unaoongezwa makali na sera za Trump za kizalendo za "Marekani kwanza".
Mataifa ya SCO huenda yakajadili uwezekano wa eneo huru la kibiashara la pamoja, alisema , wakati China pia inajaribu kusukuma ushiriki katika mradi wake wa miundo mbinu ya ukanda na barabara ya dunia.
"Mataifa wanachama wa SCO wanataka mafanikio ya juhudi za ukanda huo na barabara pamoja na kuongezeka kwa ushawishi wa China ikiwa kama nguvu kuu
No comments