MTOTO FANYIWA UKATILI WA KUCHOMWA MOTO MAKALIO
Mtoto mwenye umri wa miaka {11}amechomwa moto makalioni na kufungiwa ndani kwa muda wa siku mbili kwa kosa la kuiba pesa kiasi cha shilingi elf tano kitendo ambacho ni cha kikatili katika maisha yake .
Mtoto huyo anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Mwinyi iliyopo mkoani Tabora jina limehifadhiwa amefanyiwa ukatili huo siku ya jumatatu ya tarehe 11 /06 /2018 akiwa kwa baba yake mdogo wilayani kahama.
Akizungumza na kituo hiki Mtendaji wa mtaa wa nyihogo Bwn.Antony Costa amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti pamoja na majirani wa familia hiyo na kuwa mtuhumiwa wa kosa hilo bado hajakamatwa
'Nilipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa na majirani na ndiponilipofika eneo la tukio na mtuhumiwa hajakamatwa "alisema Costa. .….
Pia msemaji wa Dawati La Jinsia wilayani Kahama mkoani shinyanga Bi . Jenny Joakim Eras amekili kupokea tukio la mtoto huyo ofisi kwake na kuwa mtoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama .
Eras ametoa ushauri kwa wanajamii kuwa na malezi bora kwa watoto woa kwa kuzingatia sheria ya mtoto ya mwaka 2009. .
No comments