Heade

WATAFITI WATOA ELIMU KWA MAAFISA KILIMO WA KATA WILAYANI TARIME


Watafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha miwa na mazao ya mizizi kutoka kibaha mkoani pwani wametoa mafunzo kwa afisa kilimo wa ngazi za kata katika wilaya ya Tarime mjini na Tarime vijijini juu ya magonjwa na wadudu waharibifu wa zao la mihogo.
Watafiti hao wameeleza magonjwa yanayoathiri kwa sehemu kubwa kuwa ni Batobato, Michirizi ya kahawia na Vidonda ikiwa wadudu waharibio mazao hayo ni Utitiri na Nzi mweupe huku wakitaja aina ya mbegu za  mihogo   inayokomaa haraka na kutoa mavuno mengi.
Mkurugenzi wa almashauri ya wilaya ya Tarime Apoo Castrol Tindwa amewapongeza watafiti hao kwa jitihada na kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka maafisa kilimo wa kata kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata huku wakihakikisha wanayafikisha katika kata zao ili kuwawezesha wakulima kuzui na kukabiliana na magonjwa pamoja na wadudu waharibifu.

Naye afisa kilimo wa almashauri ya wilaya ya Tarime Bw Silvanus Gwiboha amewashukuru watafiti na waelimishaji hao kuleta mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya maendeleo ya kilimo cha mihogo kwa wakulima.

No comments

Powered by Blogger.