BARICK IMEKUBALI MASHARTI YOTE YA SHERIA MPYA YA MADINI
Serikali imesema kampuni ya madini ya Barick imekubali masharti yote ya sheria ya mpya ya madini pamoja na kulipa Dola za marekani millioni 300 sawa na shilingi billionni 660kwaajili ya kuonesha uaminifu.
Hayo yamesemwa leo ikilu jijini Dar es salaam na waziri wa sheria na katiba PROF PALAMAGAMBA KABUDI wakati akitoa mrejesho wa kamati maalum iliyoundwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwaajili ya kufanya majadiliano na wawakilishi kutoka kampuni ya Barick.
Aidha amesema kuwa kampuni hiyo imekubali kujenga maabara na kiwanda cha kuchakata makinikia nchini na kuachana na wafanyakazi wa mkataba bali kuajiri wazawa ambao hawatakuwa wanakaa kambini.
Naye mwenyekiti mtendaji wa Barick John Thomas amesema kuwa makubaliano hayo yataenda kuidhinishwa na bodi nchini Uingereza ambayo ina hisa asilimia 64.
No comments