MARUFUKU KUAGIZA TRANSFOMA NGUZO NA VIFAA VINGINE VYA UMEME KUTOKA NJE YA NCHI
Waziri wa nishati Dk Medard Kalemani amepiga
marufuku kwa shirika la umeme TANESCO na wakala wa umeme vijijini REA kuacha
kuagiza transfoma ,nguzo na vifaa vingine kutoka nje ya nchi ili kudhibiti
uingizwaji holela wa vifaa visivyo na ubora vinavyoathiri na kudidimiza uchumi
wa ndani.
Ametoa rai hiyo baada ya kutembelea kiwanda cha
kutengenezea transfoma TANALEC kilichopo jijini Arusha amesema serikali imepata
hasara kubwa kwa uingizwaji wa transfoma kutoka nje ambapo hivi karibuni zaidi
ya transfoma 20 ziliingizwa hapa nchini na kugundulika kuwa ziko chini ya
kiwango.
Mkurugenzi wa TANALEC Zahri Salehe amesema
wanajipanga kuzalisha Transfoma za kutosha ili kumudu soko la ndani huku naye
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali ya mkoa huo
itahakikisha inasimamia utekelezaji wa agizo hilo.
No comments