MNANGAGWA ATARAJIWA KUAPISHWA KUWA RAIS WA ZIMBABWE
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye kufutwa
kazi kwake kulichochea mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe na kupelekea jeshi
kuchukua udhibiti wa madaraka
anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya Robart Mugabe aliyeiongoza nchi hiyo kwa muda mrefu
kujiuzulu baada ya kuwepo kwa maandamano
ya wananchi wa Taifa hilo wakishinikiza aachie ngazi hali iliyochochewa na kile
kinachodaiwa kuwa alitaka kumrithisha kiti hicho mke wake bi Grace Mugabe.
Mnangagwa amesema kipaombele chake ni kujenga upya uchumi
wa nchi hiyo na kuunda ajira mpya kwa idadi kubwa ya watu wasio na ajira na
kulishukuru jeshi la nchi hiyo kuliingilia kati baada ya baada ya yeye
kufukuzwa na rais Robart Mugabe.
No comments