TANESCO WATAKIWA KUWAFUATA WANANCHI VIJIJINI.
WAZIRI Mkuu,
Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liwafuate
wananchi walioko katika vijiji vinavyotarajiwa kuunganishiwa umeme kupitia
Wakala wa Nishati Vijijini REA.
Amesema
serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika
vijiji vyote ambavyo havijaunganishiwa nishati hiyo nchini, hivyo ni vema
wakawatembelea wananchi katika maeneo yao na kuwahudumia.
Waziri Mkuu
ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara
katika uwanja wa michezo Tunduru huku akiwasisitiza watumishi wa TANESCO
kutokaa maofisini na badala yake wakawahudumie wananchi katika maeneo yao.
Amesema
serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote
nchini, vikiwemo vya wilaya ya Tunduru ambapo wananchi hao wataunganishiwa
umeme huo kwa gharama ya Sh 27,000 tu.
No comments