Heade

EWURA IMETANGAZA ONGEZEKO LA BEI ZA REJAREJA NA JUMLA YA MAFUTA

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati EWURA imetangaza ongezeko la bei za rejareja na jumla kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli kuanzia novemba MOSI mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa EWURA  mhandisi Godwin  Samwel amesema ongezeko hilo kwa bei ya jumla linatokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia.
Petroli imeongezeka kwa shilingi 55 kwa lita moja  sawa na asilimia 2.69 , dizeli shilingi 46  sawa na asilimia 2.43 na mafuta ya taa ni shilingi 81  sawa asilimia 4.35.

Ongezeko la bei ya mafuta kwenye soko la ndani imetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo kwenye soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ambayo ndiyo fedha inayotumika kununulia mafuta

No comments

Powered by Blogger.