Heade

AHUKUMIWA KWA KUOA MKE WA PILI

Mahakama nchini Pakistan imemhukumu kifungo cha miezi sita jela mwanaume mmoja kwa kosa la kuoa mke wa pili bila idhini kutoka kwa mke wake.
Mahakama hiyo ya mjini Lahore imemhamrisha mwanaume huyo kulipa faini ya dola 1900 na kukataa maoni yake kuwa dini yake inamruhusu kufanya hivyo.

Mke wa kwanza wa Shahzad anayefahamika kwa jina la Ayeshe Bibi alijitetea kuwa  mumewe alifanya hivyo bila idhini yake suala ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kifamilia nchini humo huku wanaharakati wa masuala ya wanawake wanasema kuwa kesi hiyo nipigo kwa ndoa za wake wengi.

No comments

Powered by Blogger.