ATIWA MBARONI KWA KUIBA SHILINGI 873,000
Mhasibu wa hospitali ya mkoa mjini Singida aliyeachishwa kazi kwa kosa la
kumiliki vyeti feki Edith Talasi 49 mkazi wa minga anashikiliwa na jeshi
la polisi kwa tuhuma za kuvunja milango ya ofisi yake ya zamani na kuiba
shilingi 873,000 kwa kutumia funguo bandia akiwa na mlinzi wa nyumbani kwake.
Kamanda wa polisi jeshi la polisi mkoani singida ACP Debora Magiligimba amesema
tukio hilo limefanyika novemba 21 saa sita na nusu usiku mwaka huu ambapo
amesema Edith alikamatwa akiwa amejifungia ndani ya ofisi ya muhasibu.
Amesema pamoja na wizi huo imeelezwa kwamba april mwaka huu wahasibu wa
hospitali hiyo walibaini upotevu wa shilingi milioni moja laki nane pia mwezi
octoba mwaka huu wamebaini upotevu wa shilingi milioni tatu na laki sita fedha
zilizo potea kwa mazingira ya kutatanisha.
Aidha watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na baada ya kumalizika kwa
mahojiano watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabilili.
No comments