MASHIRIKA YANAYOTETEA HAKI ZA BINADAMU YAMETAKIWA KUTOUWEKA MBALI UKATILI WA KIUCHUMI
Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Anna mghwira ameyataka
mashirika yanayotetea haki za binadamu na yanayopinga vitendo vya ukatili wa
kijinsia katika mikoa ya kanda ya kaskazini kutouweka pembeni ukatili wa
kiuchumi kwani ndio unaozaa ukatili mwingine.
Ameyazungumza hayo
akiwa katika stendi kuu ya mabasi moshi
mjini, yaendayo mikoani wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia.
Ameongeza kuwa katika uongozi wa awamu ya tano mhe, rais
Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha anapambana kumaliza ukatili
wa kiuchumi katika migodi ya madini na dhahabu kwani rasilimali za nchi
zilikuwa hazimnufaishi mwananchi.
Amewataka watu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu
kuzungumzia suala la ukatili wa kiuchumi.
Maaadhimisho hayo yanaratibiwa na shirika la kilimanjaro women information exchange and comunity organisation yakihusisha mikoa ya kilimanjaro,Arusha, Tanga,na Manyara ambayo hufanyika kila mwaka.
No comments