MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Abdalah
Malela amemvua madaraka Mwalimu Mkuu Masunga Ng’waya wa Shule ya Msingi
Mwashagata, iliyopo kijiji hicho kata ya Ihusi kwa kosa la ukosefu wa
maadili.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, mkurugenzi huyo alisema
tukio hilo lilitokea hivi karibuni la baada ya mwalimu mmoja wa shule
yake kumrubuni mwanafunzi wake kwa kufanya mapenzi naye tena kwenye
nyumba yake, kitendo ambacho ni cha kukosa maadili.
“Imebainika hili ni tukio la nne kwa mwalimu huyo kutuhumiwa kufanya
mapenzi na wanafunzi tofauti tofauti lakini amekuwa hachukuliwi hatua,
lakini mimi kwa mujibu wa sheria nimemvua madaraka mwalimu mkuu huyo ili
awe mwalimu wa kawaida, sababu amekosa maadili ya kuendelea kushika
wadhifa huo,” alisema mkurugenzi huyo.
Aidha, alisema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote
mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine, Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisikitishwa na kitendo hicho na
kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumchukulia hatua na kuwashauri
wazazi wamuache mwanafunzi huyo aendelee na masomo yasije yakampita huku
hatua za kisheria kwa mtuhumiwa zikiendelea.
Mlezi wa mwanafunzi huyo, alisema mwanawe alisimama masomo kwa muda
wa wiki mbili kutokana na tukio hilo. Mwalimu Ng’waya alipozungumza na
mwandishi wa habari kwa njia ya simu alikiri kuvuliwa madaraka na
kueleza amekuwa mwalimu wa kawaida huku akiendelea kufundisha katika
shule hiyo
No comments