Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amesema raia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani
na kusaidiwa kurejelea maisha ya kawaida.
Akizungumzia video za
karibuni ambazo zimekuwa zikiwaonesha Waafrika wakiuzwa kwenye mnada wa
watumwa nchini Libya, Rais Buhari amesema inasikitisha sana kwamba
"baadhi ya raia wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi - dola kadha Libya".
Ameonekana
pia kushangaa iwapo raia wa Libya walijifunza lolote la maana tangu
kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
''Walichojifunza
pekee ni kuwapiga watu risasi na kuua. Hawakujifunza kuwa mafundi wa
umeme, mafundi wa mabomba au ufundi wowote ule," amesema.
Kwenye
video iliyotolewa na CNN mapema mwezi huu, vijana kutoka mataifa ya
Afrika kusini mwa jangwa la Sahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi
wa mashambani kwa wanunuzi.
Walikuwa wanauzwa $400 (£300) katika eneo ambalo halikufichuliwa Libya.
No comments