Kikao cha kusikiliza rufaa
iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague,
Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa washtakiwa kusema
amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu.
Slobodan Praljak, 72,
alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa
Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika mahakamani.
Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni "eneo la uhalifu".
Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar.
Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, "Nimekunywa sumu".
Sita
hao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa unatolewa
na mahakama maalum ya kimataifa ya UN iliyokuwa inashughulikiwa makosa
yaliyotekelezwa Yugoslavia (ICTY).
Ingawa walikuwa washirika dhidi
ya Waserbia wa Bosnia wakati wa vita hivyo vya 1992-95, Wacroatia wa
Bosnia na Waislamu walipigana wenyewe kwa wenyewe kwa miezi 11.
No comments