WANANCHI RORYA WATAKIWA KULIMA KILIMO CHA MHOGO
Wananchi wa wilaya rorya wametakiwa kulima zao la muhogo baada ya kupatiwa mbegu zinazokinzana na magonjwa ambayo yamekuwa yakishambulia zao hilo huku wilaya hiyo ikitajwa kutegemea zao hilo kwa asilimia 30 ya chakula.
Hayo yameelezwa na afisa kilimo wa wilaya ya Rorya Bw. Dominick Ndyetabula katika maadhimisho ya siku ya Mkulima wa muhogo kanda ya ziwa hivi karibuni ambayo yamefanyika wilaya ya rorya katika kijiji cha Masanda kata ya Ikoma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka wilaya za serengeti ,Biharamulo, Ngara, Sengerema ,Magu na Rorya.
Kwa upande wake afisa kilimo Mkowa wa Mara Denis Ngaya amesema kuwa mkoa wa mara zao la muhogo limekuwa ni tegemezi kubwa mbali na kushambuliwa na magonjwa mbalimbali lakini serikali inaendelea na jitihada za kupatikana kwa mbegu kinzani ili kuongeza uzalishaji.
Katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Simon Chacha akiwa kama mgeni rasmi ametoa wito kwa viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji , vijiji na kata kuendelea kuhimiza wananchi kulima zao hilo la muhogo litakalokuwa mkombozi kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo.
No comments