WATU 8 WAPOTEZA MAISHA MJINI NEW YORK
Meya wa mji wa newyork Bill De Blasio amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo.
Aidha bwana Bill amelielezea tukio hilo kuwa la kigaidi ambalo limesababisha hofu mjini humo ambapo amesema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.
Kwa upande wao polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi,mtuhumiwa wa tukio hilo amechukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao wamethibitisha taarifa hizo katika kituo cha lower manhattan.
No comments