Heade

UCHAFUZI WA MAZINGIRA BADO NITATIZO KUBWA NCHINI

Uchafuzi wa mazingira kutokana na mifuko ya plastiki jijini dar es salaam na maeneo mengine nchini bado ni tatizo kubwa huku ikielezwa kuwa asilimia 90 ya uchafu wa bahari ya hindi unatokana na mifuko hiyo.
Waziri wa nchi,ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh Januar Makamba amesema maamuzi ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo nchini hayawezi kufanywa na wizara yake pekee.
Mh Makamba amesema uamuzi juu ya jambo hilo unahusu idara na taasisi za serikali na sekta binafsi hivyo uamuzi wa pamoja kutoka katika idara na taasisi za serikali na sekta binafsi ndio utakuwa dawa ya kukomesha utengenezaji,uagizaji na matumizi ya mifuko hiyo nchini.
Aidha mbali na uchafuzi wa mazingira waziri huyo amesema mifuko hiyo inapokaa kwenye maji kwa muda mrefu husagika na kuwa katika chembe chembe ndogondogo ambazo huliwa na samaki.

Na kutokana na hali hiyo watu hula chembechembe hizo za mifuko pale wanapokula samaki hao, lakini pia mifuko hiyo ina madhara kwa mifugo kama vile ng'ombe ambao hufa wanapoila mifuko.

No comments

Powered by Blogger.