Heade

WAZAZI WAMETAKIWA KUWAPA MOYO WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

Wazazi wa wanafunzi wa kidato cha pili wilayani Rorya wametakiwa kuwatia moyo na  kuwahasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi kwani masomo hayo ni mhimu kuelekea Tanzania ya viwanda na  uchumi wa kati. 
Hayo yamesemwa na Afisa elimu wa wilaya ya Rorya Gabriel Paulo wakati akizungumza na redio Sachita ofisi kwake na kuongeza kuwa jamii ya Rorya inatakiwa kusaidia watoto wa kike kuepuka mimba zinazopelekea kukatisha masomo yao.
Aidha amesema kuwa kwa wilaya ya Rorya watahiniwa wa kidato cha pili  ni elfu tatu na mia saba sabini na nane wakiume wakiwa elfu  moja mia nane tisini na saba na wa kike elfu moja mia nane themanini kwa shule zote 32 za sekondari  wilayani humo.
Pia ameiomba serikali na wadau wa maendeleo kusaidia kuboresha miundo mbinu ya vyumba vya vya madarasa, mabweni pamoja na maabara ili kuwafanya wanafunzi wajifunze masomo ya sayansi kwa urahisi.


No comments

Powered by Blogger.