Heade

SERIKALI IMEWASILISHA MSWADA WA SHERIA KUANZISHA SHIRIKA JIPYA LA MAWASILIANO

Serikali imewasilisha muswada wa sheria ambao unaiua rasmi  kampuni ya simu Tanzania TTCL na kuanzisha shirika jipya la mawasiliano Tanzania ambalo litamilikiwa na serikali kwa asilimia 100
Muswada huo umewasisilishwa bungeni jana na waziri wa Ujenzi,Uchukuzi, na Mawasiliano prof Makame Mbarawa huku wabunge wakipinga baadhi ya vifungu vya Muswada huo.

Prof Mbarawa. amesema madhumuni ya muswada huo ni kuanzisha shirika hilo kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma kikamilifu kwa jamii na kuongeza kuwa sheria hiyo mpya itawezesha TTCL kutekeleza majukumu yake kama shirika la umma la mawasiliano litakalojulikana kama Tanzania Telecommunication Corporation.

No comments

Powered by Blogger.