IMEELEZWA kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini inatokana na jamii
kutokuwa na elimu ya afya ya uzazi inayochangiwa na umaskini ambapo
mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa anazaa watoto zaidi ya nane.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile
“Takwimu za utafiti wa hali ya afya na idadi ya watu mwaka 2015/2016
inaonyesha kasi ya ongezeko la idadi ya watu ni 2.7 na hali ya uzazi ni
wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke aliye kwenye umriwa kuzaa,’’
alisema Ndugulile.
Alisema wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke asiye na elimu ni watoto
saba, wakati kwa mwanamke aliyefikia elimu ya sekondari ni watoto wanne
na wale walio na hali ya umaskini mama anazaa watoto nane
ikilinganishwa na yule mwenye uchumi mzuri anayezaa watoto watatu.
Alisema serikali ya awamu ya tano inahakikisha mtoto anayetakiwa kwenda
shule kwa ngazi ya msingi na sekondari inagharamia elimu yao .
Aliongeza serikali inasisitiza ujenzi wa viwanda ili vijana wanaomaliza
masomo ngazi mbalimbali wapate ajira.Mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini,
Jacqueline Mahon, alisema kumekuwapo na ongezeko kubwa la kutokuwa na
usawa duniani la kipato, rasilimali na haki.
Alisema katika nchi nyingi zilizoendelea ikiwamo Tanzania, wanawake
wengi wanakosa nguvu katika kufanya maamuzi juu ya masuala ya afya ya
uzazi, ikiwamo juu ya maamuzi ya muda na wakati gani wa kushikaujauzito.
“Usawa na ustawi wa watu wote ni msingi wa malengo ya maendeleo endelevu
ya dunia ili kuyafikia, tunahitaji kuwajengea uwezo wale
ambaowanaonekana wako nyuma hasa wanawake na watoto wa kike,” alisema.
Cristina Kwayu, kutoka UNFPA, alisema kila mwaka idadi ya watu
inaongezeka ambapo kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na watu zaidi ya
milioni 50.
Aliongeza kuwa changamoto ya kasi ya idadi ya watu imechangia watoto
kutopelekwa shule, mtoto kuzaa mtoto hata madarasa kutojitosheleza
kutokana na kila mwaka watoto kuongezeka.
No comments