Heade

POLISI MKOANI RUKWA YAMSHIKILIA MCHINA KWA KUINGIZA MASHINE KINYEMELA

POLISI mkoani Rukwa inaendelea kumshikilia mwekezaji raia wa nchi ya China Yi Huang (27) ambaye amelipa faini ya Sh milioni 12 ikiwa ni gharama ya kuteketeza mashine 41 za michezo ya kubahatisha zikiwa na thmani ya Sh milioni 41.

Mashine hizo ambazo hazijasajiliwa na mamlaka husika zilingizwa kinyemela nchini kutoka nchi jirani ya Zambia pia mshtakiwa alipopekuliwa alikutwa na sarafu za fedha za Zambia Kwacha ambazo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.

Pia mshtakiwa huyo alikutwa pia na sarafu za mia mbili zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili zilizokuwa zikitumika kuchezesha kamari kupitia mashine hizo. Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kimelipwa kupitia amana ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ambao maofisa wake wakaguzi walizikamata na kuziteketeza .

"Mshtakiwa huyu tunaendelea kumshikilia ila tunashikilia pia hati yake ya kusafiria hadi hapo atakapowasilisha leseni yake ya biashara… Kaka yake ambaye mshtakiwa anadai ndiye mwenye mali hizo amesafiri kwenda nchini China ambapo anatarajiwa kurejea nchini baada ya wiki tatu ....

Yi ana Viza daraja la kwanza ambayo inamtabulisha kama mwekezaji hana tatizo lolote la uhamiaji " alieleza Kyando . Akifafanua alieleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi na maofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha kwa kushirikiana na askari polisi ambapo walizikamata mashine 41 za kuchezea kamari ambazo zilikuwa zimefichwa katika nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Majumba Sita nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga .

No comments

Powered by Blogger.